๐ Maswali na Majibu (FAQs) - Wosomtz.online
Karibu kwenye sehemu ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu huduma zetu za Wosomtz.online. Tafadhali soma hapa chini:
1. Wosomtz.online ni tovuti ya aina gani?
JIBU: Wosomtz.online ni jukwaa la kidigitali kwa ajili ya kutangaza kazi za wasanii – nyimbo, video, picha na maudhui mengine ya ubunifu. Zinapatikana kwenye injini za utafutaji kama Google, Bing, Yahoo n.k.
2. Nawezaje kuweka kazi yangu kwenye Wosomtz.online?
JIBU: Tunapokea kazi zako kupitia email au WhatsApp. Tembelea ukurasa wa Mawasiliano kwa maelezo zaidi.
3. Naweza kutuma kazi kupitia WhatsApp?
JIBU: Ndiyo, tuma kama Document (Nyaraka) kwa ubora zaidi.
4. Mnazipokea nyimbo za aina gani?
JIBU: Tunapokea nyimbo/video zote zenye maadili, kutoka kwa wamiliki halali au wawakilishi walioidhinishwa.
5. Kuna malipo yoyote msanii hupata akichapisha kazi yake?
JIBU: Hapana. Huduma zetu ni bure. Hatuuzi muziki au maudhui ya msanii kwa mtu wa tatu.
6. Kazi yangu ikichapishwa, inaweza kusaidia views kwenye YouTube, Boomplay, au Audiomack?
JIBU: Ndiyo. Tunatumia embed code kutoka kwenye akaunti zako rasmi. Watazamaji wanaelekezwa moja kwa moja huko.
Note: Hatuhusiki na malipo, hesabu za viewers au sera za tovuti kama YouTube, Boomplay n.k.
7. Nifanyeje nikiona mtu ametuma wimbo wangu bila ruhusa?
JIBU: Tuma maelezo kupitia email peterkamwaya8@gmail.com. Tutaufuta ndani ya masaa machache ikiwa utathibitisha kuwa wewe ndiye mmiliki halali.
๐ข Faida za Kuweka Muziki Wako Wosomtz.online
- Unaonekana kwenye Google, Bing, Yahoo n.k
- Zaidi ya maelfu ya watembeleaji kila mwezi
- Kazi zako zinasambazwa kwenye mitandao ya kijamii moja kwa moja
- Watembeleaji wanaweza kudownload au kusikiliza kazi zako moja kwa moja